Habari za siku ya inne asubuhi tarehe 15/06/2023
- Kulifunguliwa jana mjini Lubumbashi kikao cha kumi na nane DRC Mining Week, yani wiki ya madini inchi Kongo yakidemokratia. Mada ni "Tambua ushindi wa sekta ya madini nchini DRC "
- Jimboni Kivu ya Kusini, Shirika ya kiraia inaelezea wasiwasi wake kuhusu kazi ya mradi ya maendeleo ya mitaa mia moja na makumi inne na tano katika jimbo hilo.
- Katika jimbo la Kivu ya Kusini, visa vingi vya nyumba kuwaka moto katika mji la Bukavu si vya uhalifu lakini ni kwa kutokuwa makini .
- Katika mji wa Goma, mwanabunge Prince Kihangi anamuomba liwali wa jimbo kusimamisha kazi ya ujenzi ya uzio wa gereza kuu la Munzenze.
- Daktari kiongozi wa Kituo cha Usambazaji Damu mjini Butembo anaalika watu wa moyo mwema kutoa damu yao ili kuokowa maisha ya wengine.
- Na mjini Beni, watu watano watoaji bora wa damu kwa miaka mengi, walipewa vieti na heshima siku ya tatu hii katika sherehe ya Siku kuu ya Wachangia Damu Duniani.
- Katibu Mkuu makamu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na suala la ubakaji unaofanywa wakati wa migogoro anayepatiakna mjini Goma tangu siku ya pili, alitembelea siku ya pili hiyo , Hospitali ya Heal Africa mjini Goma.
- Muungano wa kitaifa wa vyama vinavyopigana dhidi ya mimba zisizotamaniwa unaomba kuondowa adhabu kuhusu jambo la kuondowa mimba nchini kongo ya kidemokratia kufuatana wa azimio ya Maputo.
- Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini: mwanamke ambaye alishtakiwa kuua mtoto, alihukumiwa kwa azabu ya kifo siku ya pili na mahakama ya kijeshi ya mji wa Goma./sites/default/files/2023-06/15062023-p-s-journalswahilimatingraceamzati-00_web_.mp3