Habari za jioni 28 Aprili, 2025
- Kinshasa : Zaidi ya watu makumi mbili wamekufa kwa kipindu pindu inchini Kongo kwa wiki iliyopita. Wizara ya afya ilitangaza hayo Siku ya tano iliyopita wakati wa baraza la mawaziri, ikiongeza kwamba ni kati ya Wagonjwa zaidi ya elfu moja waliorekodiwa
- Goma : Huko Kivu Kaskazini, kundi lenye kumiliki silaha la Coalition des patriotes résistants congolais-Force de frappe, Pareco-FF, kwa kifupi, linashutumiwa kwa vitendo vya unyanyasaji dhidi ya raia pa Katoyi katika tarafa la Masisi
- Bandundu : Shirika la Umeme nchini, SNEL kitengo cha Bandundu kubwa, linaomba serikali ya mkoa wa Kwilu kulinda kituo chake cha umeme cha Tobakita ambacho vifaa vyake viliharibiwa na wanamgambo wa Mobondo. /sites/default/files/2025-04/280425-p-s-jounalswahilisoir-00-web.mp3