Journal Soir

Habari za jioni 16 Aprili, 2025

  • Kinshasa : Kitengo cha dharura ya mafuriko mjini Kinshasa na majimbo mengine ya Kongo kimewekwa ili kutathmini kiwango cha hali na kuchukua hatua za haraka. Kikao kilifanyika kwa ajili hiyo hii siku ya pili mjini Kinshasa chini ya uongozi wa rais wa Jamuhuri
  • Beni : Ubelgiji inathibitisha uungaji mkono wake kwa Kongo kuhusu hali ya usalama inayoendelea mashariki mwa inchi. Balozi wa Ubelgiji nchini Kongo alisema hayo huko Beni hii siku ya pili ambako alipokelewa na liwali wa jimbo
  • Bunia : Wanabunge wa kijimbo wa Ituri wanaomba mishahara yao ilipwe, na kuomba uongozi wa kijeshi ukomeshwe, wakizani kwamba umeshindwa kurejesha usalama huko./sites/default/files/2025-04/160425-p-s-journalswahilisoir-00-web.mp3