Habari za jioni 19 Februari, 2025
- Beni : Mapigano makali yaliendelea hii siku ya tatu tarehe kumi na tisa Februari, kati ya waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda, na jeshi la FARDC katika maeneo tofauti tarafani Lubero jimboni Kivu Kaskazini
- Lubumbashi : Zaidi ya kesi elfu moja mia tano na tano za Ugonjwa wa kipindupindu zikiwemo vifo makumi tatu na saba zimerekodiwa tangu mwanzoni mwa mwaka katika jimbo la Haut Katanga
- Bandundu : Katika jimbo la Kwango, wanyama pori wanaharibu mashamba ya wakulima katika tarafa la Kasongolunda, tangu mda sasa. Msimamizi wa eneo hilo anasema ametoa ripoti kwa wakuu wake ili kuchukua hatua dhidi ya hali hiyo./sites/default/files/2025-02/190225-p-s-journalswahilisoir-00-web.mp3