Habari za jioni 13 Februari, 2025
- Goma: Waasi wa M23 walikutana hii siku ya tatu na mameneja wa benki, na taasisi Ndogo za fedha katika kikao, kwa lengo la kuanza kwa shughuli za benki katika jiji la Goma huko Kivu Kaskazini
- Bunia: Huko Ituri, wakazi wengi wa vijiji vinavyoshambuliwa na wanamgambo wa CODECO wamekimbiya katika kambi zinazolindwa na askari jeshi wa MONUSCO katika tarafa la Djugu
- Bandundu : Hali ya malisho mabaya ya kiwango cha juu inazingatiwa tangu mda mrefu katika tarafa la Kasongolunda, hasa katika sekta ya Panzi, katika jimbo la Kwango./sites/default/files/2025-02/130225-p-s-journalswahilisoir-00-web.mp3