Habari za siku ya tatu jioni tarehe 21/12/2022
- Azimio la kuondoa utaratibu wa kutoa taarifa za kuuza vifaa vya kijeshi na usaidizi kwa serikali ya Kongo ilipitishwa kwa kauli moja.
- "Rwanda lazima ikomeshe uungaji mkono wake kwa M23, Ufaransa inalaani uungaji mkono wake kwa kundi hili lenye silaha. Uhusiano ambao tumeujenga upya na Kigali, tutauweka katika huduma ya amani”.
- Katika Kivu Kaskazini, karibu watu makumi tano wakiwemo wanawake na watoto wadogo wamekamatwa tangu siku ya kwanza na waasi wa M23 huko Mulimbi, Mudugudu na Rusekera.
- Shughuli ya kuwatambua na kuwasajili wapigakura itaanza siku ya sita hii, tarehe makumi mbili na ine Desemba.
- Kuhusu Mchakato wa uchaguzi, makamu wa kwanza wa mkuu wa tume huru ya taifa ya uchaguzi, Bienvenu Ilanga alithibitisha siku ya pili tarehe makumi mbili Desemba mwaka tunao, kuandaa shughuli za utambuzi na uandikishaji wa wapiga kura katika maeneo yaliyokumbwa na ukosefu wa usalama, hususan katika tarafa la Bagata katika jimbo la Kwilu na lile la Kwamouth huko Mai-Ndombe.
- Katika Equateur Kubwa, Tofauti na mzunguko wa uchaguzi wa mwaka elfu mbili kumi na nane, CENI wakati huu inatumia zaidi wasadizi wa kijamii, ili kuhamasisha wapigakura. Wakiwa na t-shirt, kofia, mabango na ujumbe mwingine, lazima watavuka miji na vijiji, mlango kwa mlango.
- Katika jimbo la Maniema, ni tangu tarehe kumi na tano Desemba ambapo kampeni ya kuzuia homa kali ilizinduliwa huko Maniema.
- Tuko mwezi Desemba, sherehe za mwisho wa mwaka zimekaribia. Hapa Kinshasa, tunaona ishara nyingi zaidi hapa na pale. Baadhi ya barbara kuu za zimepambwa, ni mpango wa serikali ya mkoa wa jiji la Kinshasa./sites/default/files/2022-12/21122022-p-s-journalswahilisoir-00_web_.mp3