Habari za siku ya tatu jioni tarehe 31/07/2024
- Makao ya GLM ya Rais wa zamani wa Jamhuri yakidemokratia ya Kongo, Joseph Kabila yalishambuliwa leo hii na kundi la vijana waliokuwa wamejihami kwa silaha za kienyeji.
- Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, shughuli mbalimbali za ukumbusho wa "mauaji ya halaiki ya Kongo" au GENOCOST zitaanza kesho siku inne tarehe mmoja mwezi wa mnane
- Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, hali ilikuwa ya mzozo leo siku ya tatu asubuhi kwenye barabara ya Katoyi, wilaya ya Kasika, kaskazini mwa mji wa Goma.
- Shirika la Kiraia linaohusika na kutetea Haki za Kiuchumi na Kijamii (DESC) kwa kifupi unakaribisha kutiwa saini kwa makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Rwanda na Jamhuri yakidemokratia ya Kongo, chini ya uangalizi wa Rais wa Angola, Joao Lourenço.
- Huko Ituri, askari wawili wa jeshi la Kongo FARDC waliuawa na wengine waliojeruhiwa. Hii ni matokeo ya muda ya mashambulizi ya watu wenye silaha ambao ni wa kikundi cha Zaire zidi ya nafasi za jeshi la majini huko Kasenyi , Tchomia na Sabe, kwenye pwani ya Ziwa Albert
- Jimboni Tanganyika, shirika la kiraia la mtaa wa Manono linashutumu unyanyasaji wa huduma za serikali kwenye barabara mbalimbali , hasa kwenye barabara ya Manono - Kabongo na barabara ya Manono - Lubumbashi ambapo vizuizi kadhaa vimewekwa
- Katika jimbo la Kivu ya Kusini, liwali wa jimbo alikutana jana mjini Bukavu na ma kampuni ya uchimbaji madini yanayotumika katika jimbo hilo.
- Katika jimbo la Tshopo, viama via wavuvi vilipokeya vifaa kutoka kwa Waziri wa Uvuvi na Mifugo ili kuboresha kazi yao ya uvuvi.
- Watu wawili wanaozaniwa kuwa wale waliosabibisha matokeo mabaya ya uwandja Martyrs siku ya sita iliyopita wakati wa sherehe ya mwimbaji Mike Kalambay walikamatwa nakupelekwa mahakami./sites/default/files/2024-07/310072024_-_journalswahilisoirgraceamzati-00_web.mp3