Journal Soir

Habari za siku ya pili jioni tarehe 30/07/2024
 

  • Watu makumi mbili walifariki na wengine wengi kupotea :  haya ni matokeo ya muda ya kuzama kwa mashua ndogo siku ya mungu jioni huko KAMBOLÉ mjini Kindu katika jimbo la Maniema. 
  • Katika jimbo la Kivu ya kusini, Moto uliwaka siku ya pili hii  katika kituo cha mafuta huko Bukavu karibu na hospitali kuu ya Bukavu. Matokeo  ya muda ni  watu watatu kujeruhiwa  vibaya, nyumba mbili, magari mawili na pikipiki mbili zilizochomwa moto.
  • Jimboni Kivu ya kaskazini, mradi wa STAR-EST, ambao ni mradi wa Uimarishaji na ukarabati  wa barabara Mashariki mwa Kongo ulizinduliwa siku kwa kwanza Mjini Beni .
  • Hapa mjini Kinshasa, ujumbe wa Benki ya Dunia, ukiongozwa na Mkurugenzi wake anayehusika na operesheni , Bwana  Albert Zeufack, uliwasilisha siku ya kwanza kwa Waziri wa Elimu , Raissa Malu, mfuko yakukuza elimi unayokadiriwa kwa  dolla za marekani milliari mmoja na nukta inne. 
  • Huko Ituri, soko la UZI lililoko kilomita makumi kenda  na tatu kaskazini mwa Bunia katika eneo la PIMBO mtaani Djugu linafanya limeanza tena kutumikishwa baada ya miaka sita ya kufungwa kwake kufuatia unyanyasaji ya makundi yenye kumiliki  silaha. 
  • Jamuhuri ya Kidemokratia ya Kongo inashutumu Rwanda kwa kuvuruga mawasiliano yake ya anga ambayo kulingana na viongozi wa Kongo inahatarisha usalama wa usafiri wa anga nchini. 
  • Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, utulivu ulionekana siku ya pili  hii huko Katwe, katika eneo la Mutanda , usulutani wa Bwito mtaani  Rutshuru baada ya mapigano kati ya waasi wa m23 na wapiganaji kutoka kundi la CMC/FAPC la  Jonas Bigabo usiku wa wakuamkiya siku ya pili hii.
  • Hali imekuwa ya wasiwasi  kwa siku tatu katika eneo la magharibi la la Bashali Mokoto, mtaani Masisi.
  • Wafanyakzi wa Kampuni ya Usafiri ya Kongo (Transco) wanaamua  kusitisha mgomo wao siku ya pili hii , baada ya kulipwa kwa mishahara yao ya miezi miwili na Waziri wa Fedha.
  • Usafiri  hapa Kinshasa umerejea kama  kawaida katika sehemu kubwa ya mji ./sites/default/files/2024-07/30072024-s-journalswahilisoirgraceamzati-00_web.mp3