Habari za siku ya tano jioni tarehe 26/07/2024
- Katika mtaa wa Beni jimboni Kivu ya kaskazini, idadi ya watu waliouawa wakati ya mashambulizi ya waasi wa ADF huko Babila-Bakaiko siku ya tatu na siku ya inne inaongezeka kutoka takriban watu makumi mbili hadi watu makumi tano.
- Katika jimbo la Ituri, takriban watu kumi na watano wamekamatwa na waasi wa ADF na wakulima wengi moja wamekimbia vijiji vyao na shughuli za mashambani huko Lolwa katika usulutani wa Babila Bakwanza mtaani Mambasa.
- Umoja wa Ulaya unaweka vikwazo yani adhabu dhidi ya watu kenda
- Huko Maniema, viongozi wanawake wa shirika liitwao Rien Sans les Femme wanapaza wanashutumu kutokuwepo kwa wanawake katika serikali jimboni ya Liwali Moussa Kabwankubi Moise.
- Katika jimbo la Tshopo, kuliandaliwa siku ya tatu na siku ya inne pa ISC Kisangani kikao kuhusu mwenendo ya vyuo vikuu
- Shirika la utafiti liitwao Ebuteli liliaandaa kikao jana siku ya inne hapa Kinshasa ambako shirika FONAREDD linaohusika na mazingira liliwasilisha ripoti lake la kazi
- Michezo kazaa inayoitwa Jeux Olympiques inaanza leo hii siku ya tano mjini Paris, inchini Ufaransa.Kunakuwa piya wachezaji wanaowakilisha Jamhuri yakidemokratia ya Kongo
- Kuhusu tu michezo hii, tuwajulishe kwamba Brigitte Mbabi na Arnold Impelenga ndio watawakilisha ujumbe wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa sherehe yakufungua michezo hii leo mjini Paris/sites/default/files/2024-07/26072024-s-journalswahilisoirgraceamzati-00_web.mp3