Habari za siku ya tano jioni tarehe 12/07/2024
- Serikali ya Kongo inaomba jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua kali dhidi ya Rwanda na viongozi wake, ambao wanajeshi wao wanaopatikana nchini Kongo pia wanashambuliya wanajeshi wa
- Jimboni Kivu ya Kaskazini, mapigano yanaendelea leo hii siku ya tano kati ya waasi wa M23 na kundi mmoja lenye kumiliki silaha katika eneo la Bashali Mokoto mtaani Masisi.
- Katika jimbo hilo la Kivu ya Kaskazini, tuwajulishe kwamba askari wa jeshi la Kongo FARDC, aliyehusika na mauaji ya msichana mdogo na majeraha ya risasi katika kambi ya wakimbizi ya Lushagala, pia aliuawa na watu wenye hasira.
- Suala la Mobondo katika mtaa wa Kwamouth jimboni Mai-Ndombe: mapigano makali yalitokea hapo siku ya tatu kati ya jeshi na wanamgambo hao ambao walifukuzwa.
- Mjini Kinshasa, maiti ya dereva wa teksi iligunduliwa leo asubuhi mbele ya offisi wa Kukuza Viwanda, Fpi, karibu na ubalozi wa Marekani.
- Katika jimbo la Tshopo, viongozi wa mitaa wanashutumu kutolipwa kwa mishahara yao.
- Zaidi ya wiki moja baada ya kuanza kwa operesheni yakumaliza kabisa teksi ya pikipiki katikati mwa mji wa Lubumbashi, hali inabadilika mjini.
- Jimboni Kivu ya Kusini, maji ya Regideso kwa mara nyingine tena yanatoka katika sehemu kubwa ya mji wa Bukavu baada ya zaidi ya wiki mbili ya ukosefu wa maji ya kunywa./sites/default/files/2024-07/12072024-p-s-journalswailisoirgraceamzati-00_web.mp3