Journal Soir

Habari za siku ya pili jioni tarehe 09/07/2024

  • Hali ya usalama mashariki mwa Kongo yakidemokratia inazungumziwa katika kikao cha makumi inne na kenda cha Bunge linalozungumza Kifaransa ambacho kilifunguliwa tarehe tano mwezi huu wa saba huko Montreal, inchini Canada.
  • Kukomeshwa  kwa vita mashariki mwa Kongo  hakutawezekana kama  Rwanda na washirika wake wa M23 wanaendelea kuleta vurugu  na viongozi wa Rwanda kutoheshimu ahadi zao kihusiana na mchakato wa Luanda . Maelezo ya Balozi  wa Kongo kwa Umoja wa Mataifa.  
  • Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, shirika ya kiraia, linaamini kuwa usimamizi wa vita kwaajili ya usaidizi wa kibinadamu hautakuwa na matkokeo mazuri  kama waasi wa M23 wataendelea kuchukuwa nakuzibiti   maeneo Kongo.
  • Shirika lakuteteya haki za binadamu liitwao la Voix de Sans Voix, linaomba  jumuiya ya kimataifa kulazimisha Rwanda kuondoa  wanajeshi wake katika inchi la  Kongo.
  • Hali ya kibinadamu katika jimbo la Ituri inahitaji  suluhisho ya kudumu,  haswa kurejea kwa wakimbizi  katika vijiji vyao . Maneno haya yalitolewa siku ya kwanza  na mratibu wa masuala ya kibinadamu, BRUNO LEMARQUIS ambaye yuko huko Ituri.
  • Mjini  Kinshasa, mtu mmoja  mfanyakazi ku shirika ya usalama ANR alipigwa risasi na kuuawa nyumbani kwake siku ya pili hii, kwenye makutano ya barabara za Lititi na Lokolo, katika eneo la  Matadi Kibala  mtaani Mont-Ngafula. 
  • Katika  mtaa wa Lubero jimboni Kivu ya Kaskazini, wanajeshi makumi na wawili wa FARDC wanahukumiwa adhabu ya kifo na mahakama ya kijeshi ya Butembo.
  • Washtakiwa watatu wa Kimarekani katika kesi ya jaribio la mapinduzi ya madaraka  la tareha kumi na kenda mwezi wa tano uliyopita  wanaomba kuachiwa kwa mshtakiwa mwenza wao wa Ubelgiji Jean-Jacques Wondo.
  • Jimboni  Kasai-Oriental , zaidi ya nyumba mia moja zilizojengwa kiholela kwenye eneo linanayojulikana kwa kawaida Mitembela katika  mtaa wa Kanshi, mjini Mbuji Mayi, zitabomolewa siku zijazo./sites/default/files/2024-07/090724-p-s-journalswahilisoirgraceamzati-00_web_1.mp3

Dans la même catégorie