Journal Soir

Habari za siku ya pili jioni tarehe 04/04/2023 

  • Katika jimbo la Ituri, watu kumi na mmoja walipoteya kwa  kuzama kwa boti siku ya kwanza  kwenye Mto Ituri kwenye  sehemu ya Beni-Mambasa.
  • jimboni  Kivu ya Kusini, mtumbwi ilizama katika maji ya Ziwa Kivu na kuua watu sita, manusura yani waliookolewa makumi mnane na karibu watu makumi sita ambao walikuwa walipoteya hadi wakati huu.
  • Jimboni Kivu ya Kaskazini: hesabu ya watu waliofariki katika  maporomoko ya udongo wikendi iliyopita, katika eneo la Bulwa, mtaani  Masisi, inaongezeka . Inatoka kwa watu makumi mawili  na moja hadi makumi mawili  na watano waliofinikwa  na maporomoko ya mawe.
  • Nchini Congo, kuna hesabiwa maeneo makumi matatu zenye kuwemo hatari za miripuko za bomu hasa zaidi katika jimbo la Kivu ya kaskazini. Kiungo cha SILAM chenye kuhusika kinasema kwamba ni hasara kwa masiha ya wakaAJI. Ndivyo imesemwa leo siku ya kukomesha hali hiyo duniani kote. 
  • Jimboni Kivu ya Kaskazini, kikosi cha Uganda cha EAC hatimaye kiliwekwa rasmi jana siku ya kwanza huko Bunagana.
  • Katika jimbo la Lomami, Barabara ya Taifa namba mbili inayounganisha miji ya Kabinda na ile ya Mbuji Mayi imekatwa vipande viwili katika  kijiji cha Musengie, karibu kilomita makumi tatu  na nne kutoka Kabinda.
  • Mtoto yeyote mwenye ulemavu wa aina yoyote lazima asaidiwe katika kiwango cha kisaikolojia na kuzingatiwa kama mtoto mwingine yeyote anayeitwa kuwa na uwezo wa kufanya kazi.
  • Bunge la jimbo la Kongo central linamshukuru mkuu wa nchi kwa kutimiza ahadi yake aliyoitoa kwa waumini wa kanisa la Kimbangu  tarehe sita mwezi wa inne mwaka wa elfu mbili makumi mbili na moja  wakati wa sherehe  ya miaka mia moja  ya kanisa la Kimbangu katika mji mtakatifu wa Nkamba   kwa kuweka tarehe sita mwezi wa inne kama siku isiyo ya kazi na ya kulipwa katika jamhuri nzima./sites/default/files/2023-04/040423-p-s-kinjournalswahilisoir-00_web.mp3