Journal Soir

Habari ya siku ya pili jioni tarehe 10 /10/2023

  • Baada ya kufungwa kwa shughuli ya kupokea na maombi ya uchaguzi wa urais wa  mwaka huu, baadhi ya waangalizi wanazumza kuhusu  mpamgo  ya uchaguzi . Ni kama vile Profesa Bob Kabamba, mwalimu wa Chuo Kikuu cha Liège nchini Ubelgiji, ambaye anadhani kwamba kalenda hii inakuwa na shida ya kwamba,   orodha ya mwisho ya wagombea itatangazwa tarehe kumi na mnane mwezi wa kumi, yani  siku moja kabla ya kuanza kwa kampeni za uchaguzi. .
  • Kwa kujibu, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa CENI anathibitisha kwamba hiyi ni shida inaopatikana katika sheria ya uchaguzi.
  • Katika jimbo la Kasai Oriental,  kulifanyika  makabidhiano ya siku ya kwanza  kati ya kamati inayoingia na hiyo inaotoka ya kampuni ya uchimbaji madini ya Bakuanga MIBA.
  • Katika jimbo la Kongo Central, waziri jimboni wa uchumi anapinga kupanda kwa  bei ya sakafu  ambayo inazingatiwa siku hizi mkoani humo.
  • Katika Kivu Kaskazini – yapata magari makumi mawili  yaliyokuwa yamebeba bidhaa na abiria yaliokwama kwa wiki moja huko Nturo na Kitshanga katika eneo la Bashali Mokoto, katika mtaa wa  Masisi, yaliachiliwa na kuendelea na safari hadi siku ya kwanza  kuelekea mji wa Goma.
  • Huko Mjini  Goma, siku moja baada ya mahakama ya kijeshi kutoa hukumu za wafuasi wa dini la wazalendo , maoni kadhaa yanaripotiwa.
  • Na Huko Ituri, kumekuwa  ukosefu wa maji ya kunywa kwa karibu  mwezi mmoja katika usulutani wa Babila Babombi, ambalo lina zaidi ya wakaazi elfu miya tatu  , wakiwemo wakimbizi  wa vita.
  • Katika jimbo la Tshopo, wahami wa  mzozo wa jamii ya Mbole_Lengola walio kwenye eneo la parokia ya Ste Marthe ya  Lubunga wanaomba msaada wa kibinadamu kutoka kwa serikali na  washirika wake./sites/default/files/2023-10/101023-p-s-kinjournalswahilisoir-00_web.mp3