Habari za siku ya kwanza asubuhi ya tarehe 19/06/2023
- Jeshi la Uganda linatoa wito kwa wakazi wa Bwera kuwa waangalifu na kushutumu adui yoyote katika maeneo yao.
- Baada ya shambulio hili la waasi wa ADF, wa shule katika eneo la Uganda jirani na mji wa Kasindi wa Kongo Ya Kidemokratia, wanajeshi wa FARDC wanasema wako waangalifu kwa ajili ya usalama wa mji huu wa mpakani na wakazi wake.
- Lawama na kushutumu shambulio hili la waasi wa ADF kwenye shule nchini Uganda zanatoka kote ulimwenguni.
- Jimboni Ituri, majaribio kadhaa ya mashambulizi ya makundi yenye kumiliki silaha yalizuiwa wiki iliyopita na jeshi la Monusco katika mtaa wa Djugu.
- Katika jimbo la Ituri tuwajulishe kwamba, zaidi ya watu elfu kumi na mbili wahami walipokeya wiki inayopita msaada wa vifaa vya nyumbani katika maeneo ya Mwanga na Kunda, karibu kilomita kumi kaskazini mwa Bunia.
- Rais Félix-Antoine Tshisekedi alielezea wasiwasi wake kufuatia kuzorota kwa hali ya kuunda biashara katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
- Miezi sita kabla ya uchaguzi, , Rais wa zamani Joseph Kabila baada ya kimya kwa muda mrefu anaanza mawasiliano na wanamemba wa chama chake cha kisiasa.
- Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, wafanyabiashara wa mafuta, wanakubaliana tena juu ya malipo wa ushuru wa kawaida wa ujenzi katika jimbo hilo./sites/default/files/2023-06/190623-journalswahilimatingraceamzati-00_web_.mp3