Journal matin

Habari za siku ya tano asubuhi tarehe 16/06/2023

  • Ni leo hii tarehe kumi na sita mwezi wa sita ndio kunasherekwa Siku kuu ulimwenguni ya Mtoto wa Afrika . Jimboni Ituri, zaidi ya  watoto elfu makumi mawili  na moja  hawaendi shule kwa sababu ya vita  inayoathiri jimbo hili.
  • Ni siku ya inne hii ndio mitihani ya Kitaifa la Uchaguzi, Mwelekeo wa Kielimu na Kitaalamu, TENASOSP ilianza .
  • Huko jimboni Maniema, liwali  wa muda AFANI IDRISSA MANGALA ndiye aliyezindua mitihani hii kutoka shule ya msingi kindu ville mbele ya viongozi kazaa  wa jimbo hili.
  • Katika jimbo la Equateur ,  liwali makamu na liwali wa muda  alialika siku ya inne hii  wanafunzi wenye kufanya mitihani  wa kitaifa wa ya TENASOSP kukimbiza  woga. Lakini kutumika  kwa utulivu. Kwa hivyo, watafaulu katika mitihani hii .
  • Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini,  Timu  ya kuunga mkono mpito hadi kuondoka kwa taratibu kwa Monusco inchini Kongo Iliwekwa rasmi jana mjini Goma.
  • Mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa CPI anatangaza kwamba atafanya uchunguzi ya kwanza  kuhusu uhalifu wa "majeshi na makundi yenyi kumiliki silaha " katika jimbo la Kivu Kaskazini
  • Kufuatana na kikao la kumi na nane la wiki ya madini ya Kongo yakidemokrasia, shirika la maendeleo la Marekani linasema liko tayari kusaidia Kongo  kukuza sekta yake ya madini.
  • Katika jimbo la Ituri, zaidi ya visa elfu moja na mia tano vya surua vimeripotiwa katika muda wa miezi minne katika eneo la afya la Nia-nia, yapata  kilomita mia tatu kutoka mji wa Bunia  mtaani Mambasa.
  • Jimboni Kivu ya Kusini,  kampeni  dhidi ya ugonjwa wa kiumbe cha kizazi ilizinduliwa siku ya tatu hii mjini Bukavu. /sites/default/files/2023-06/160623-p-s-journalswahilimatingraceamzati-00_web.mp3