Journal Matin

Habari z'asubuhi 30 Aprili, 2025

  • Kinshasa :   Makubaliano ya kanuni yaliyotiwa saini na Kongo na Rwanda chini ya uangalizi wa Marekani, ni hatua katika mwelekeo sahihi. Rais Felix Tshisekedi alisema hivyo hii siku ya pili akijibu swali la mwandishi wa habari wakati wa mkutano na waandishi wa habari aliyouandaa mjini Kinshasa
  • Goma : Tarehe makumi tatu aprili, Siku ya Elimu nchini Kongo, ni siku ya giza kwa walimu wanaoishi katika maeneo yaliyokaliwa na waasi wa M23. Katika maeneo yanayokaliwa katika Kivu Kaskazini walimu bado hawajapokea mishahara yao tangu mwezi Januari mwaka huu tunao kutokana na kutopatikana kwa benki
  • Lubumbashi : Jimboni Lualaba, polisi waliwasilisha week end hii, kundi la watu wanaoshukiwa kuwa majambazi wenye silaha kwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa jimbo huko Kolwezi. Miongoni mwa watu hao kuna kamanda mmoja wa polisi./sites/default/files/2025-04/300425-p-s-journalswahilimatin-00-web.mp3