Habari z'asubuhi 01 Aprili, 2025
- Kinshasa : Mfuko wa Kitaifa wa Fidia kwa Wahasiriwa wa Unyanyasaji wa Kijinsia Unaohusiana na Migogoro (FONAREV) ulianzisha Mazungumzo juu ya utambuzi wa mauaji ya kimbari ya Kongo hii siku ya kwanza tarehe makumi tatu na moja Machi mjini Kinshasa
- Goma : Wafanyakazi wa serikali katika jimbo la Kivu Kaskazini ambao bado hawako Beni, mji mkuu wa muda wa jimbo hilo, wamepewa likizo ya kiufundi kutokana na tukio la kipekee ambalo haliwezi kukabiliwa. Habari ambayo haiingii vizuri katika masikio yao
- Bandundu : Kampeni za uchaguzi wa maliwali, makamu wa maliwali na maseneta wa jimbo la Kwilu, iliyoanza tarehe makumi mbili na tisa Machi, zinaendelea kama kawaida hadi sasa. Uchaguzi huo unakuja baaya ya kurudishwa nyuma kutokana na vurugu za Yakoma na Kwilu./sites/default/files/2025-03/010425-p-s-journalswahilimatin-00-web.mp3