Habari z'asubuhi 25 Februari, 2025
- Kinshasa : Hali ya usalama na kibinadamu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imefikia kiwango cha kutisha. Judith Suminwa, Waziri Mkuu wa Kongo alisema hayo hii siku ya kwanza katika kikao cha Baraza la Haki za Kibinadamu huko Geneva
- Goma : Katika Jimbo la Kivu Kaskazini, timu ya Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, PAM, na washirika wake wameanza tena usaidizi wa chakula kwa sehemu, katika baadhi ya maeneo ya jiji la Goma
- Kinshasa : Mfanya biashara Mike Kasenga ameachiliwa huru hii siku ya kwanza na Cassation katika kesi ya uchimbaji maji. Mahakama inasema hakupatikana na hatia ya wizi wowote./sites/default/files/2025-02/250225-p-s-journalswahilimatin-00-web.mp3