Habari z'asubuhi 20 Februari, 2025
- Bunia : MONUSCO haikujenga mahema mia nane huko Bunia ili kuwapokonya silaha wanajeshi wa FARDC endapo mji huo utashambuliwa na wanajeshi wa Uganda. Monusco na jeshi la Kongo ndo wamejibu hivyo kutokana na habari za uongo zinazosambaa kuhusu suala hilo
- Bandundu : Liwali wa mda wa Kwilu Jean Mallaut Mbongompasi, anaonya wakazi wanaojifanya wakimbizi ili kunufaika na misaada ya wakimbizi wa kweli pa Bandundu
- Lubumbashi : Zaidi ya kesi elfu moja mia tano na tano za Ugonjwa wa kipindupindu zikiwemo vifo makumi tatu na saba zimerekodiwa tangu mwanzoni mwa mwaka katika jimbo la Haut Katanga/sites/default/files/2025-02/200225-p-s-journalswahilimatin-00-web.mp3