Journal Matin

Habari z'asubuhi 14 Februari, 2025

  • Kinshasa : Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, CPI, imeonyesha nia yake ya kuwawajibisha wale wote waliohusika na vita mashariki mwa Kongo. Uhakikisho huo umetolewa na naibu mwendesha mashtaka wa mahakama hii, Mame Mandiaye Niang
  • Kalemie : Huko Kalemie, takriban visa mia moja vya kipindupindu vikiwemo kifo kimoja vimerekodiwa katika mitaa ya afya ya Kalemie na Nyemba. Kutumia maji ya Ziwa Tanganyika na Mto Lukuga yasiyowekewa dawa ndo chanzo, wanasema viongozi wa afya wa pahali
  • Kinshasa: Siku ya redio duniani ya kila tarehe kumi na tatu februari iliadhimishwa jana siku ya ine chini ya mada Redio na mabadiliko ya hewa./sites/default/files/2025-02/140225-p-s-journalswahilimatin-00-web.mp3