Habari z'asubuhi 13 Februari, 2025
- Kinshasa : Ujumbe wa Baraza la Maaskofu wakatoliki la CENCO na Kanisa la Kristo nchini Kongo (ECC) walikutana jana siku ya tatu mjini Goma na Corneille Nanga pamoja na viongozi wengine wa kundi la waasi la M23 ili kuitoa nchi katika mgogoro inayoipitia
- Kinshasa : Kesi kati ya Kongo na Rwanda imefunguliwa hii siku ya tatu tarehe kumi na mbili februari mbele ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu pa Arusha, inchini Tanzania
- Mbandaka ; Jimboni Equateur, Seneta Boketshu Bofili Jean Paul anaonya kuhusu kuibuka kwa ugonjwa usiojulikana ambao umeenea katika tarafa la Basankusu na kusababisha vifo vya makumi ya watu katika muda wa chini ya wiki moja./sites/default/files/2025-02/130225-p-s-journalswahilimatin-00-web.mp3