Journal matin

Habari za siku ya tatu asubuhi tarehe 31/07/2024
 

  • Hali ya usalama na amani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ilizungumziwa jana wakati wa majadiliano kati ya  Rais wa Angola , João Lourenço na wakuu wa masuala ya indje wa Kongo, Rwanda na Angola. 
  • Jamuhuri ya Kidemokratia ya Kongo inashutumu Rwanda kwa kuvuruga mawasiliano yake ya anga ambayo kulingana na viongozi wa Kongo inahatarisha usalama wa usafiri wa anga nchini. 
  • Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, utulivu ulionekana siku ya pili  hii huko Katwe, katika eneo la Mutanda , usulutani wa Bwito mtaani  Rutshuru baada ya mapigano kati ya waasi wa m23 na wapiganaji kutoka kundi la CMC/FAPC la  Jonas Bigabo usiku wa wakuamkiya siku ya pili hii.
  • Jimboni Kivu ya kaskazini, mradi wa STAR-EST, ambao ni mradi wa Uimarishaji na ukarabati  wa barabara Mashariki mwa Kongo ulizinduliwa siku kwa kwanza Mjini Beni .
  • Huko Ituri, soko la UZI lililoko kilomita makumi kenda  na tatu kaskazini mwa Bunia katika eneo la PIMBO mtaani Djugu linafanya limeanza tena kutumikishwa baada ya miaka sita ya kufungwa kwake kufuatia unyanyasaji ya makundi yenye kumiliki  silaha. 
  • Watu makumi mbili walifariki na wengine wengi kupotea :  haya ni matokeo ya muda ya kuzama kwa mashua ndogo siku ya mungu jioni huko KAMBOLÉ mjini Kindu katika jimbo la Maniema.
  • Katika jimbo la  Kivu Kaskazini, msimamizi wa kitengo cha wa afya jimboni anaonya kuhusu mahitaji yakupata damu yanaongezeka  katika miundo ya afya ya jimbo hilo./sites/default/files/2024-07/31072024-s-journalswahilimatingraceamzati-00_web.mp3