Journal matin

Habari za siku ya tano asubuhi tarehe 19/07/2024

  • Kuanzia sasa, mhusika yeyote wa makosa yanayohusiana na ujenzi haramu, uvamizi wa mifereji ya maji na  kelele atalipa  faini ya hadi sawa na dola mia tano. Hii ni matokeo ya kikao cha kazi kati ya Waziri wa Sheria na Waziri Mjumbe wa Wizara ya Mipango ya ujenzi wa Miji na Makazi siku ya tatu.
  • Moto mkubwa ulijitokeza siku ya tatu  jioni mjini  Mbandaka na kuaribu karibu maduka kumi na tano, na  dola elfu kadhaa
  • Jimboni Nord-Ubangi, mtaa wa Yakoma kwa sasa inakuwa na zaidi ya familia mia tatu za wafugaji wa Mbororo, na maelfu ya ng'ombe wao.
  • Kipindi cha kusimamisha mapigano kwa ajili ya msaada ya kibinadamu katika mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kimeongezwa kwa siku kumi na tano zaidi na serikali ya Marekani
  • Mashuhuri mmoja kutoka kusini mwa Lubero anaomba kufunguliwa kwa shughuli za kibinadamu kati ya maeneo ya Lubero e na sehemu ya kaskazini ya  mtaa wa Rutshuru huko jimboni Kivu ya Kaskazini.
  • Muungano ya  Wanawake wa Amani na Usalama nchini Kongo, unaokutanisha  vyama na mashirika kadhaa ya wanawake nchini humo, ulikutana siku ya tatu  mjini Luanda na rais wa Angola.
  • MONUSCO inaunga mkono jeshi la FARDC ili  kukomesha kuendelea kwa waasi wa M23 na kukomesha unyanyasaji wa ADF ambao ni tishio kwa  majimbo ya Kivu ya Kaskazini na Ituri.
  • Kushuka kwa maji wa Ziwa Tanganyika na Mto Lukuga katika wiki za hivi karibuni.
  • Sehemu ya barabara ya taifa namba makumi tatu, RN30 kati ya mji wa Uvira inchini Kongo na Bujumbura nchini Burundi inaanza kutumika tena baada ya maji ya Nyangara kando ya Ziwa Tanganyika kupungua./sites/default/files/2024-07/190724-journalswahilimatingraceamzati-00_web.mp3