Habari za siku ya tatu asubuhi tarehe 10/07/2024
- Hali ya usalama mashariki mwa Kongo yakidemokratia inazungumziwa katika kikao cha makumi inne na kenda cha Bunge linalozungumza Kifaransa ambacho kilifunguliwa tarehe tano mwezi huu wa saba huko Montreal, inchini Canada.
- Kukomeshwa kwa vita mashariki mwa Kongo hakutawezekana kama Rwanda na washirika wake wa M23 wanaendelea kuleta vurugu na viongozi wa Rwanda kutoheshimu ahadi zao kihusiana na mchakato wa Luanda . Maelezo ya Balozi wa Kongo kwa Umoja wa Mataifa.
- Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, shirika ya kiraia, linaamini kuwa usimamizi wa vita kwaajili ya usaidizi wa kibinadamu hautakuwa na matkokeo mazuri kama waasi wa M23 wataendelea kuchukuwa nakuzibiti maeneo Kongo.
- Shirika lakuteteya haki za binadamu liitwao la Voix de Sans Voix, linaomba jumuiya ya kimataifa kulazimisha Rwanda kuondoa wanajeshi wake katika inchi la Kongo.
- Hali ya kibinadamu katika jimbo la Ituri inahitaji suluhisho ya kudumu, haswa kurejea kwa wakimbizi katika vijiji vyao . Maneno haya yalitolewa siku ya kwanza na mratibu wa masuala ya kibinadamu, BRUNO LEMARQUIS ambaye yuko huko Ituri.
- Mjini Kinshasa, mtu mmoja mfanyakazi ku shirika ya usalama ANR alipigwa risasi na kuuawa nyumbani kwake siku ya pili hii, kwenye makutano ya barabara za Lititi na Lokolo, katika eneo la Matadi Kibala mtaani Mont-Ngafula.
- Katika mtaa wa Lubero jimboni Kivu ya Kaskazini, wanajeshi makumi na wawili wa FARDC wanahukumiwa adhabu ya kifo na mahakama ya kijeshi ya Butembo.
- Washtakiwa watatu wa Kimarekani katika kesi ya jaribio la mapinduzi ya madaraka la tareha kumi na kenda mwezi wa tano uliyopita wanaomba kuachiwa kwa mshtakiwa mwenza wao wa Ubelgiji Jean-Jacques Wondo./sites/default/files/2024-07/100724-p-s-journalswahilimatingraceamzati-00_web.mp3