Habari za siku ya tatu asubuhi ya tarehe 05/04/2023
- Hali mbaya ya kibinadamu katika jimbo la Kivu Kaskazini, Shirika lisilo la Kiserikali la Medecins sans frontieres, linatoa wito wa usaidizi.
- Nchini Congo, kuna hesabiwa maeneo makumi matatu zenye kuwemo hatari za miripuko za bomu hasa zaidi katika jimbo la Kivu ya kaskazini.
- Liwali wa jimbo la Kivu ya Kaskazini anafurahishwa na juhudi zilizofanywa na majeshi ya Kongo na Uganda katika operesheni za pamoja za "SHUJAA" dhidi ya waasi wa ADF katika eneo la Beni.
- Katika jimbo la Ituri, watu kumi na mmoja walipoteya kwa kuzama kwa boti siku ya kwanza kwenye Mto Ituri kwenye sehemu ya Beni-Mambasa.
- jimboni Kivu ya Kusini, ambako mtumbwi ilizama katika maji ya Ziwa Kivu na kuua watu sita, manusura yani waliookolewa makumi mnane na karibu watu makumi sita ambao walikuwa walipoteya hadi wakati huu.
- Jimboni Kivu ya Kaskazini: hesabu ya watu waliofariki katika maporomoko ya udongo wikendi iliyopita, katika eneo la Bulwa, mtaani Masisi, inaongezeka . Inatoka kwa watu makumi mawili na moja hadi makumi mawili na watano waliofinikwa na maporomoko ya mawe
- Katika jimbo la Lomami, Barabara ya Taifa namba mbili inayounganisha miji ya Kabinda na ile ya Mbuji Mayi imekatwa vipande viwili katika kijiji cha Musengie, karibu kilomita makumi tatu na nne kutoka Kabinda.
- Mtoto yeyote mwenye ulemavu wa aina yoyote lazima asaidiwe katika kiwango cha kisaikolojia na kuzingatiwa kama mtoto mwingine yeyote anayeitwa kuwa na uwezo wa kufanya kazi.
- Bunge la jimbo la Kongo central linamshukuru mkuu wa nchi kwa kutimiza ahadi yake aliyoitoa kwa waumini wa kanisa la Kimbangu tarehe sita mwezi wa inne mwaka wa elfu mbili makumi mbili na moja wakati wa sherehe ya miaka mia moja ya kanisa la Kimbangu katika mji mtakatifu wa Nkamba kwa kuweka tarehe sita mwezi wa inne kama siku isiyo ya kazi na ya kulipwa katika jamhuri nzima./sites/default/files/2023-04/05042023-p-s-kinjournalswahilimatingraceamzati-00_web.mp3