Habari za siku ya tatu asubhi tarehe 21/12/2022
- Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilifanya upya siku ya pili mamlaka ya Monusco nchini DRC kwa mwaka mmoja
- Rais wa Jamhuri Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo anasubiriwa siku ya tatu hii tarehe makumi mbili na moja Desemba mjini Mbandaka ili kuongoza kongamano la tisa la magavana litakaloanza siku ya ine tarehe makumi mbili na mbili Desemba.
- Mjini Kinshasa, ibada ya pamoja kwa ajili ya waathiriwa wa mvua kubwa iliyonyesha siku ya pili tarehe kumi na tatu Desemba iliandaliwa hii siku ya pili kwenye uwanja wa ikulu ya raia. Rais wa Jamhuri akisindikizwa na Mke wake, Waziri Mkuu, wajumbe wengi wa serikali na wawakilishi wa familia za wahanga walishiriki katika ibada hii.
- Huko jimboni Kivu ya Kusini, hali ya kijamii na kiuchumi inazidi kuwa ngumu katika tarafa la Kalehe, wakati sherehe za mwisho wa mwaka tunao zinakaribia.Katika jimbo la Kasai Oriental, bei ya vyakula vingi pamoja na bidhaa za viwandani imepanda kwenye soko la Mbuji-Mayi.
- Katika Kivu Kaskazini, viongozi wa eneo wa usultani wa Bukumu katika tarafa la Nyiragongo wanapeana hekta makumi tatu kwa jumuiya ya kibinadamu.
- Watu wanane wanaodaiwa kuwa ni wezi walichomwa moto wakiwa hai katika muda wa wiki mbili katika mji wa Kalemie. Kulingana na mkuu wa vuguvugu la kiraia la Parlement debout sans Tabous ambaye alitoa habari hii siku ya pili kwa Redio Okapi, hali hii ya kusikitisha inatokana na kutokuwepo kwa doria za polisi. Kwa Nathan Mugisho, vijana kutoka vitongoji wanajipanga ili kujilinda.
- Kuhusu uandikishaji wa wapiga kura katika jimbo la Kwilu. Zaidi ya vituo elfu moja mia ine vya kujiandikisha vimepangwa kwa ajili ya utambuzi na uandikishaji wa wapigakura utakaoanza tarehe makumi mbili na ine Desemba.
- Katibu Mtendaji wa Mkoa wa Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi ya Kongo central, alisema yuko tayari kwa shughuli ya utambuzi na uandikishaji wa wapigakura, kwa mujibu wa kalenda ya uchaguzi iliyotangazwa hivi karibuni na kiongozi wa kitaifa wa taasisi hii ya kusaidia demokrasia.
- Chama cha kisiasa cha Ensemble pour la République kinaandaa kongamano lake siku ya pili mjini Lubumbashi. Uzinduzi wa kazi za kongamano hilo umetolewa leo asubuhi na mkuu wa chama hiki, Moise Katumbi./sites/default/files/2022-12/21122022-p-s-journalswahilimatin-00_web_.mp3