Jounal Matin

Habari z'asubuhi 24 Mach, 2025

  • Kinshasa : Serikali ya Kongo inasubiri kuona uasi wa AFC/M23 kutimiza klwa vitendo uamzi wake wakuondoa vikosi vyake Walikale na kandokando. Waziri wa mambo ya inje wa Kongo alisema hivyo siku ya sita akijibu katika mkutano aliyouandaa na waandihsi wa habari mjini Kinshasa
  • Kinshasa : Mjini Kinshasa, Mashauriano ya kisiasa kuhusu kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa yataanza hii siku ya kwanza tarehe makumi mbili na ine Machi. Ofisi ya Mshauri Maalum wa Mkuu wa Nchi kuhusu Usalama ndo ilitangaza siku ya sita wakati wa mkutano na waandishi wa habari
  • Mbuji-Mayi : Huko Kasai Oriental, mvua iliyonyesha siku ya sita jioni ilisababisha uharibifu mkubwa katika mji wa Mbuji-Mayi. Makumi ya nyumba yaliporomoka./sites/default/files/2025-03/240325-p-sw-journalswahilimatin-00-web.mp3