" Serkali ya jimbo ni nini, na kazi yake ni gani ? "

Fichier audio : téléchargez Flash pour écouter.

” SERKALI YA JIMBO NI NINI, NA KAZI YAKE NI GANI ? “.
rn* Serkali ya jimbo ni shina lenyi kuwa na madaraka ya utendeji katika jimbo.Kufatanananukta 198 ya Kura ya jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo,serkali ya jimbo inao viongozi hivyo.liwali wajimbo na makamu wake na mawaziri wa jimbo.
Liwali na makamu wake wanachaguliwa kwa mda wa miaka mitano,yakurudilia kwa mara moja na wateuli wa baraza la abunge jimboni wenyi kuwa ndani aoa nje ya baraza la abunge lile.Wanao madaraka kutokana na dikriti ya raisi wa jamuhuri.

” NI NANI MWENYI KUWA NA MADARAKA YA KUWATAJA MAWAZIRI WA MAJIMBO ? ”

* Mawaziri wa majimbo wanatajwa na liwali wa jimbo kati ya wanamemba wa bunge la jimbo ao nje ya bunge. Idadi yao haiwezi kupita mawaziri kumi.Inafaa kujulisha kama kuundwa kwa serkali ya jimbo.kunafatana na ginsi jimbo linawakilishwa kufatana na mitaa.
Mbele ya kuchukua madaraka yake .liwali wa jimbo anajulisha bunge la jimbo mpango wa kazi zake. Wakati mpango wakazi zake unakubaliwa na wateule wa jimbo kwa uwingi, hao watawashimika madarakani mwao mawaziri wa majimbo .
Kwa upande ungine inafaa tujue kama mawaziri wa majimbo kwa jumla ao kwa upekee wanawezwa kuondoshwa madarakani mwao kulingana na maoni iliyochaguliwa na wateule wa majimbo.

” HATAU GANI HUENDA KUCHUKUA IKIWA KAMA LIWALI WA JIMBO ANAFARIKI, AO ANAONDOSHWA MADARAKANI, ANAZUHILIWA KWA MDA MREFU AO PIA ANASTAKIWA ? ”

* Nukta 160 ya sheria sifuru sita,kistari sifuru sifuru sita ya tarehe kenda mwezi watatu mwaska wa elfu mbili na sita kuhusu matayarisho ya uchaguzi wa uraisi, wa wateule wa taifa na wale wa majimbo, wamiji mikibwa ,mitaa na lokaliti, sheria hiyo inahakikisha kama ikiwa kama liwali wa jimbo anapatikana katika hali ilitoka kutaja pale juu nin kusema , anafariki , anajihuzuru, anao kizuhizo cha mno ao kama anastakiwa , serkali ya ajimbo inapashwa kuacha madarakarn Serkali ya ajimbo ,chini ya auongozo wa liwali makamu huenda kuendelea nakazi kwa kutia usalama kati uongozo wa serkali kwa mda.
Kiisha siku kumi na tano Komisheni ya uchaguzi huru itafanyisha uchaguzi kwa kushimika serkali mpta ya jimbo.
Tujueni kama uchaguzi wa liwali wa jimbo na wamakamu wake unafanyika ikiwa kama ni nyuma mno ,kiisha siku 21,kiisha kushimikwa kwa chumba cha baraza la bunge la jimbo.
AWAZIRI WA MAJIMBO WANATAJWA NA LIWALI,WAKIWA WANAMEMBA WA BUNGE LA JIMBO AOA HAPANA.

Texte de SAMUEL KATSHAKrnOndes CourtesrnTél. : 00243998909787rnE-mail : [email protected] [email protected] Swahili de DUNIA MUKUNDA